NYAMAKA TWEVE ANIMATION

Tuesday, January 31, 2012

Spika Anne Makinda Aongoza Kikao Cha Kamati ya Uongozi Ya Bunge
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhZLCypNtwOcElZT62J7EmHhLWISiJuEDRuIqmPnvbDMz_fBnrTH53TVx3xlg4kwHrKFpuKFaaJxE6Pv555hMy92PrrRu6pg49k-76MfQCkMGmTtldp2LvREGvmv8jJbf-ZdtxF-cvAxKkC/s1600/IMG_0007.JPGSpika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) akiongoza kikao cha Kamati ya uongozi ya bunge mara baada ya kipindi cha maswali na majibu Bungeni Dodoma Leo. kamati ya Uongozi imekaa kupitia upya ratiba ya mkutano wa Bunge ulioanza leo kwa lengo la kuboresha na kupanga siku ya kujadili miswada mbalimbali itakayowasilishwa Bungeni

Saturday, January 14, 2012

PICHA ZA AJALI YA MBUGE WA CHADEMA MHESHIMIWA REGIA MTEMAAskari wa usalama barabarani mkaguzi, Kelvin Ponera akikagua gari lililopata ajali na kusababisha kifo cha mbunge wa viti maalum Chadema Mkoa wa Morogoro, Bi. Regia Mtema.


AIRTEL YAFANYA SEMINA KWA MASHIRIKA NA SEKTA MBALIMBALI NCHINI KUHUSU AIRTEL MONEY

Mkurungezi wa fedha wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Kalpesh Mehta akitoa semina ya huduma ya Airtel money kwa mashirika na wadau mbalimbali walioalikwa na kuhudhuria seminar hiyo iliyofanyika leo na kuendeshwa kwa siku mbili katika makao makuu ya Airtel , lengo likiwa ni kuwaeleimisha wafanyabiashara na mashirika mbalimbali jinsi huduma ya Airtel money inavyoweza kutoa suluhisho la matatizo yanayowapata katika kuendesha biashara zao.
Mkurungenzi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Sam Elangallor (Kushoto) akiongesha kwa vitendo jinsi gani huduma ya Airtel money inavyofanya kazi na kutoa shuluhisho kwa changamoto wanazozipata katika kuendesha biashara kwa wawakilishi kutoka katika makapuni mbalimbali waliohudhuria semina hiyo iliyofanyika Makao makuu ya Airtel, pichani anayefata ni Mkurungezi wa fedha Kalpesh Mehta na Meneja huduma Airtel money Asumpya Naligingwa.
Mkurungenzi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Sam Elangallor akitoa semina ya huduma ya Airtel money kwa wawakilishi kutoka katika makampuni mbalimbali waliohudhuria semina hiyo iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel nakuhudhuria na wadau mbalimbali na waandishi wa habari.
Mkurugenzi wa mahusiano wa Airtel Beatrice Singano Mallya akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa semina ya Airtel money inayotolewa kwa makapuni mbalimbali leo kwa muda wa siku mbili, uzinduzi huo ulifanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel na kuhudhuriwa na wadau wengi na waandishi wa habari





Wadau waliohudhuria wakichangia hoja Mmoja wa wakilishi kutoka katika makampuni yaliyohudhuria semina ya huduma za Airtel money akichangia hoja wakati wa semina hiyo iliyozinduliwa rasmi leo na kuendesha na Mkurugenzi wa Airtel Sam Ellangallor na Mkurugenzi wa fedha Kalpesh Meltha katika ofisi za makao makuu ya Airtel.


Mkurungenzi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Sam Elangallor (kushoto) na Mkurungezi wa fedha Kalpesh Mehta kwa pamoja wakitoa semina ya huduma ya Airtel money kwa wawakilishi wa makampuni mbalimbali yaliyoalikwa kupata mafunzo juu ya faida na matumizi ya huduma hiyo katika kutatua changamoto mbalimbali za uendeshaji wa biashara zao. Semina hiyo semina hiyo iliyofanyika katika makao makuu ya Airtel nakuhudhuria na wadau mbalimbali na waandishi wa habari.

-----------------------------
Katika kuhakikisha huduma ya pesa mkononi inawafikia watanzania wengi Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Leo imeendesha semina ya huduma ya Airtel money kwa wadau na sekta mbalimbali wakiwemo wadau wa usafirishaji, asasi za kifedha, wakuu wa shule na vyuo vya elimu ya juu kwa lengo la kupambanua faida za kutumia huduma mpya ya Airtel Money katika shughuli zao zinazohusiana na maswala ya kulipa au kupokea fedha.

Akizungumza wakati wa semina iliyohudhuriwa na wadau hao na kufanyika katika makao makuu ya Airtel Tanzania Afisa Mkuu wa Biashara Walingo Chiruyi alisema “lengo la semina hii ni kutaka kujadiliana na wadau wetu faida za kuitumia huduma yetu hii mpya ya Airtel Money katika shughuli zao za kila siku.

Tumegundua huduma hii ni nyenzo muhimu sana katika kuweka urahisi usalama zaidi pamoja na kupunguza hatari zinazotokana na kutembea na fedha nyingi au kukaa ofisini na fedha nyingi kwa lengo la kuzitumia katika shughuli za wiki nzima au kulipa mahitaji mbalimbali.

Airtel Money ni suluhisho la kufanya hayo yote na ndio maana leo hii tumekaa pamoja kwa lengo la kuweka kila kitu bayana kwa wadau hawa muhimu kwetu! Aliendelea kusema Bw,

Akitoa maelezo zaidi ya jinsi ya kutumia huduma ya Airtel money ambapo kwa kupitia huduma hiyo wateja wanaweza kulipa Ankra kama vile Ada ya shule, Mishahara ya wafanyakazi au vibarua, Kufanya makusanyo ya mauzo ya siku, kulipia huduma za DSTV, Luku, bili ya Dawasco, kulipia visa ya USA, pamoja na kutuma na kupokea hela ndani na nje ya nchi.

Aidha kwa wafanya biashara za usafirishaji huduma ya Airtel money itawasaidia katika kupunguza risk za wizi wa fedha na kuwaakikishia usalama madereva wakiwa safarini kwani malipo yote ya bidhaa baada ya usambazaji hayatafanyika tena kwa pesa taslimu bali kwa kupitia huduma ya Airtel money.

Kwa mabasi ya abiria wateja sasa wataweza kufanya booking na kulipa nauli kwa kupitia huduma ya Airtel money ambapo mteja hatakuwa na ulazima wa kutembelea kituo cha basi kukata tiketi na kulipia gharama za nauli.

Huduma ya Airtel money pia itapunguza gharama zilizopo katika kupata huduma za kifedha, na kwakupitia mtandao wetu ulioenea zaidi nchi nzima na mawaka waliosambaa kote tuna uhakika wa kuwafikia watanzania wengi zaidi walioko mjini na vijijini aliongeza Bi, Kazimoto.

Airtel hivi karibuni ilizindua na kuboresha huduma ya Airtel Money pesa mkononi na mpaka sasa watanzania wengi wamefaidi kwani imeweza kutoa ajira kwa watanzania wengi kwa kupitia uwakala hivyo wananchi wengi wameweza kujipatia mapato kwa kupitia huduma hii, Huduma ya Airtel money sasa ina mawakala zaidi ya 10,000 waliosambaa nchi nzima hivyo ili kukamilsha upatikanaji wa huduma hii ya kisasa na rahisi zaidi.

Posted by CATHBERT ANGELO

Friday, January 27, 2012


 

Icon

Wednesday, January 25, 2012


WATANGAZAJI, WAIMBAJI NA MAPROMOTERS WA INJILI TANZANIA WAKIJIFUA TAYARI KUPAMBANA NA TIMU YA BONGO MOVIE ITAKAYOFANYIKA JUMAMOSI, 28 JANUARY 2012

Mechi hii itachezwa katika viwanja vya TTCL/POSTA Kijitonyama (Science) ambapo kutakuwa natamasha la uimbaji baada ya mechi kuisha. Waimbaji kama Bony Mwaitege, Flora Mbasha, Bahati Bukuku, Mzee wa nyimbo ya zungukazunguka atakuwa ndani ya uwanja, na waimbaji kibao. Kutakuwa na kiingilio cha buku tano (5000/=) mlangoni, kama utataka tiketi, jisogeze maeneo ya Efatha Mwenge, Ubungo Oil Com. Mechi itaanza saa 6:00 mchna. Utakutana na waigizaji wa filamu za Kibongo kama JB, Ray, Kanuba, Irene Uwoya, Wema Sepetu, na wengine wengi.

Angalia maandalizi  haya:
Wtangazaji wa Praise Power Radio, BP (aliyekaa) na Uncle Jimmy wakijadili jambo kabla ya mazoezo kuanza
BIG..George Mpela akipiga kipenga kuwaita wachezaji uwanjani
Fuuuuuuuuulu shangwe na Bony Magupa wa macheliiiiiii...mtangazaji wa Channel Ten
Kiuno kaka..haya yalisemwa na BIG George Mpela (aliyevalia jezi ya yelow...akiwa na mzee wa mablogi Rulea Sanga (RUMA)
"Watumishi hilo zoezi ni noma..sifanyi hata kwa dawa..." Big George Mpella
Majambozi yanendelea
Mtangazaji wa Channel Ten Bony Magupa (kulia) akiwa na Mzee mzima Big-Mtangazaji wa Praise Power, George Mpella..wakitroti....
Kazi inasonga

Christabella Kombo kwa jina maaarufu Bella Kombo, hivi karibuni ameamua kuachana na muziki wa dunia na kuanza kumwimbia Bwana. Mwanadada huyo aliyeonekana kuvutia sana kwenye mashindano ya Bongo Star Seach BSS ya 2010 na 2011, hivi sasa amerekodi album yake ya nyimbo za injili. Kabla hajajiunga na Bss, Bella alikua mwimbaji mzuri kanisani na pia sauti ya Bella imesikika sana ktika baadhi ya nyimbo mbalimbali za mwalimu John Shabani.
Akiongea na mwandishi wa blog hii, bella amekiri kumrudia Bwana maana yeye siku zote alikua ni mwimbaji kanisani. Kilichotokea ni kwamba, baada ya watu na wadau mbalimbali kugundua kipaji chake, walimshauri na kumshawishi ajiunge na Bss kwamba huko kipaji chake kitajulikana zaidi pamoja na kujitangaza kwasababu kazi ya Bss ni kuinua vipaji haijalishi unaimba maadhi gani ya muziki. Baada ya kipaji chake kujulikana zaidi, alishawishiwa kujiunga na kundi la Machozi Band, hata hivyo moyo wake umekuwa ni wa kumwimbia mwenyezi Mungu. Baada ya kushauriwa na watu pamoja na watumishi mbalimbali hasa zaidi mwalimu wake bwana John Shabani ambaye hapo awali amekuwa akiimba pamoja na bella, ndipo alipoamua kurudi kundini na kuanza tena kumwimbia Bwana.
Hivi sasa Bella anategemea kujiunga na kundi la Glorious Celebration la jijini Dar es salaa