MBUNIFU WA MAVAZI KUSHIRIKI MKUTANO WA KUJADILI MASUALA YA UCHUMI DUNIANI
Mwandishi wetu
NYOTA imeanza kung’ara kwa mbunifu wa mavazi anayekuja juu kwa kasi nchini, Doreen Estazia (pichani) na lebo yake ya Estado Bird baada ya kupata kualikwa kuhudhuria mkutano wa kujadili masuala ya Uchumi duniani (World Economic Forum) utakaonza kesho mjini Devos –Klosters, Uswisi.
Estazia ambaye mwishoni mwa mwaka jana aliibuka na mavazi yaliyojulikana kwa jina la What’s Your Freedom (WYF?) kwa ajili ya kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania alisema kuwa amealikiwa kama mjasiliamali katika masuala ya ubunifu wa mavazi na atakuwa chini ya Global Shapers.
Alisema kuwa hii ni faraja kubwa kwake kwani kipaji chake ndicho kimempa nafasi hiyo na kuwa mbunifu wa kwanza nchini tokea taifa hili lizaliwe kushiriki katika mkutano huo mkubwa.
Alifafanua kuwa setka ya ubunifu wa mavazi inanulikana kimataifa kwani mbali ya kupromoti nchi nje ya mipaka na hasa masuala ya vivutio vya utalii kwa upande wa mavazi.
“Nashukuru kupata nafasi hii na nitaiwakilisha vyema Tanzania, hii ni fursa pekee ya kujitangaza kimataifa na hasa ukizingatia kuwa nimeanza kujihusisha na masuala ya ubunifu mwaka mmoja uliopita,” alisema Estazia kabla ya kuondoka juzi usiku.
Alisema kuwa ameanza kupata mwanga wa mafanikio na lengo lake kubwa ni kufikia hatua ya juu kabisa katika masuala ya ubunifu wa mavazi na wala si viginevyo.
“Sina malengo ya kuishia hapa hapa katika fani hii, nataka dunia inifahamu kupitia ubunifu wa mavazi, mkutano wa Uswis ni moja ya njia ya kufikia lengo kwani unawajumuisha pia wakuu wan chi mbali mbali duniani,” alisema.
No comments:
Post a Comment