CHRISTINA MAANDE WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B AVISHWA PETE YA UCHUMBA
Christina akionekana mnyenyekevu mbele ya kanisa na mbele ya Mchungaji wa kanisa hilo, Dkt Getrude Rwakatare baada ya kuvishwa pete na mchumba wake Jese. Dada huyu alionekana kutoa machozi kama ishara ya furaha kwa kitendo cha kupata mchumba mwenye msimamo.
Waumini walionekana kuguswa sana na tendo hilo, watu walicheza na kutoa zawadi za kumpongeza. Mama Getrude Rwakatare alionekana ni mtu aliyeguswa sana na kilio cha furaha cha Christina na hasa pale alipomvisha kitenge mchungaji wake kama ishara ya upendo.
Na sasa tuone yaliyoajili
Jese (kulia) akimsubiri mchumba wake Christina madhabahuni
Wapambe wa Bwana harusi mtarajiwa, Jese wakijiaandaa kupongeza
Wachungaji wa Mlima wa Moto Mikocheni B wakishuhudia shughuli nzima ya madhabahuni.
Kuanzia kulia ni Mama Lucas, Mch. Kyando, Mchungaji ambaye jina lake halikupatikana, Mchungaji Lukumai
Bibi harusi mtarajiwa, Christina aliyevalia orange akiwa madhabahuni na mchumba wake aliyepigilia suti kali.
Haya haya siku imewadia..Christina akiwa amepiga magoti huku akivishwa pete na mchumba wake Jese Onesmo , madhabahuni
Jese Onesmo akimshikilia kwa makini mchumba wake
Kilichofuata ni maombi makali kutoka kwa wachungaji
Mchungaji msaidizi, Lukumai (kulia) na Mchungaji Getrude Rwakatare akiwaombea wachumba hao
Mama nikupe nini.......nimempata mchumba wangu mzuri.....kilio cha furaha mbele ya mchungaji wake.
Mchungaji Getrude Rwakatare akifurahia zawadi ya kitenge kutoka kwa Christina
Haya sasa...wapambe kuvamia madhabahu kumpokea Bwana Harusi mtarajiwa
Mwimbaji mwalikwa akimwimbia Bwana wimbo wa Ebeneza
Kilio cha furaha kilitawala kwa wachumba hawa
Maombi yakiendelea
No comments:
Post a Comment