KANUMBA NYOTA ILIYOZIMIKA DUNIANI
KWA MUJIBU WA MDOGO WA MAREHEMU STEVE
KANUMBA, ALISEMA KUWA ELIZABETH MICHAEL MAARUFU KAMA LULU ALIKUJA
NYUMBANI KUKAWA NA KAUGOMVI AMBAPO WAKAINGIA CHUMBANI WAKIWA HUKO BAADA
YA MUDA,LULU ALITOKA NA KUMUITA YEYE KUMUAMBIA KANUMBA KAANGUKA, YE
ALIPOENDA AKAMKUTA KAANGUKA NDIO AKAENDA MUITA DAKTARI WA KANUMBA AMBAPO
ALIPORUDI HAKUMKUTA LULU, LAKINI HADI TUNAVYOONGEA LULU YUKO POLISI
OSTERBAY KWA AJILI YA MAHOJIANO NA POLISI, NA MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA MUCHUARI MUHIMBILI.
Watu wakiwa wamekusanyika nyumbani kwa Marehemu Stevan Kanumba.
Watu mbali mbali wakiwa wamekusanyika.
Msanii wa Bongo Movie Jackline Walper akiwa amezimia chini.
Wasanii wakiwa wameanguka na kuzimia.
Mashabiki wakiwa wamekusanyika katika
viunga vya hospitali ya Muhimbili. Habari za awali ambazo kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Kinondoni Afande Kenyela amesema kuwa Kanumba alikuwa
na kutoelewana kati yake na Mpenzi wake ambazo taarifa za awali zinasema
waligombana na Kanumba alisukumwa na kugonga kichwa chini na mpenzi
wake ambaye ametambuliwa kwa jina moja la Lulu.
Habari ambazo bado Spoti na Starehe
haijazithibitisha zinasema kuwa Kanumba alikuwa akioga ili atoke na
ndipo aliposikia mpenzi wake akiongea na simu na mtu mwingine alipotoka
kumuuliza ndipo mzozo kati yao ukaanza na katika hali ya kusumunana
Kanumba alisukumwa akaanguka na kugonga kichwa chini.
Afande Kenyela alisema alipigiwa simu na
ndugu wa Kanumba ambaye walikuwa wakiishi pamoja na Kanumba na
walipofika Pale walikuta tayari ameshakata roho ila bado inasubiriwa
ripoti ya daktari.
Kamanda Kenyela pia amesema kuwa mpenzi
wake Maerehemu Kanumba anashikiliwa na Polisi kwa uchunguzi zaidi. Lulu
ambaye naye anag’aa kwenye tasnia ya Filamu amekuwa akigonga vichwa vya
habari vya magazeti ya “udaku” kutokana na skendo za mara kwa mara za
mahusiano ya kimapenzi, ni majuzi tu mwanadada huyu ametimiza miaka 18
tangu kuzaliwa.
Aidha nyumbani kwa marehemu Sinza kumejaa
ndugu jamaa na marafiki kiasi barabara ya kwenda Lion kupitia Madukani
inapitika kwa taabu.
Kanumba ambaye alizaliwa mwaka 1984
amefanikiwa kuzikonga nyoyo za mashabiki wa tasnia ya movie za Tanzania
si tu kwa Tanzania bali hata nje ya nchi pia.
Kwa mashabiki wa filamu za kibongo Kanumba
alikuwa ni namba moja na kwa kiasi kikubwa aliweza kuweka viwango kwani
alikuwa anafaa kwa kila kona kuanzia kuigiza mpaka kuvaa na
Blogger na Graphic Designer, Rulea Sanga (mwenye njano) akitafuta matukio kwaajili yako wewe mdau wa blogu hiadamu ya
maisha tofauti na ma Super Star wengine hivyo kuwavutia watu wa rika
lote.
Nyumbani kwa marehemu
MC Nova
Ndani ya geti-nyumbani kwa marehemu
Steve Nyerere aliyevalia Polo shirt ya mistari mweusi na mweusi
Mwigizaji a.k.a Chopa Mchopanga (katikati)
Msanii wa Bongo Flava, Noora wa tatu kutoka kushoto
Mvua akinyesha, alkini watu bado wako msibani
Gari la Marehemu Steven Kanumba
Mwigizaji wa Bongo Movie aliyekuwa muongozaji wa magari na kutoa tahadhari kwa wapenzi wa marehemu
Dogo akipigwa mvua kali
Mjasiliamali, Dotnata aliyenyoosha mkono wake wa kulia akipigwa mvua msibani
Mwigizaji a.k.a Judy akihojiwa Live Channel Five
Watu hawaamini kifo cha Kanumba (jembe)
Mwigizaji Johari akilia katika mahojiano na EATV
Mwigizaji maarufu sana, a.k.a Ray aliyevalia kofia akiwasiliana na jamaa baada ya mahojiano na waandishi wa habari
Nyumbani kwa Steven Kanumba
Pia ndiye aliyewatoa watu kama Akina Wema
Sepetu, Mtoto Sophia ambaye aliigiza kwenye Movie ya Big Daddy, pia
ndiye aliyemtoa Patchou Mwamba na kumuingiza kwenye Movie Industry.
Kanumba anamaliza kipindi chake cha miaka 28 akiwa ameacha kumbukumbu
ambayo itaishi kwa muda mrefu.
Mashabiki kupitia mitandao ya kijamii
wameonyesha masikitiko yao ambapo kufika saa tisa usiku habari zilikuwa
zikisambaa kama moto nyikani kupitia Facebook, Twitter na Blogs ikiwemo
hii ya Spoti na Starehe ambayo ilikuwa moja ya wa kwanza kupata habari.
No comments:
Post a Comment