Saturday, April 7, 2012
REST IN PEACE STEVEN KANUMBA. GONE TOO SOON.
MWILI WA MAREHEMU STEVEN KANUMBA
WEMA SEPETU
NJEE YA NYUMBA YA MAREHEMU STEVE KANUMBA
MSIKILIZE MAMA YAKE MZAZI MAREHEMU STEVEN KANUMBA AKIONGEA KUHUSIANA NA TAARIFA ZA KIFO CHA MWANAE LIBENEKE NICOLAUS NGAIZA.
Flora Mtegoa mama yake marehemu Steven Kanumba akiongea na mwana libeneke wa kandayaziwaleo,
Nicolaus Ngaiza muda mfupi kabla hajapanda ndege kuelekea msibani Dar
akitokea Bukoba. Amethibitisha kupokea taarifa za kifo cha mwanae kwa
masikitiko na huzuni kubwa. Imeandaliwa na Nicolous Ngaiza, Urban Pulse
wakishirikian na Jestina George Blog
Mkurugenzi wa Global Publisher, Erick Shigongo akishirikiana na watengenezaji wa hema.
Ndani ya geti la marehemu Steven Kanumba
Blogger Rulea Sanga aliyevalia njano halkukosa msibani
H-BABA akihojiwa na waandishi wa habari
Wapenzi na ndugu wa marehemu Steven Kanumba nyumbani kwake
Mwigizaji Mainda wa pili kutoka kushoto akimfariji rafiki yake
Waigizaji wa filamu
Mwimbaji huyu alielezea jinsi alivyoaagana na Marehemu Steve Kanuba
alipohudhuria katika bendi yake siku ya jana usiku, anasema marehemu
alimtania kuwa kesho ambayo ni leo kuwa atakuja na suti kali sana ambayo
ameinunua katika bendi yake
Mjasiliamali Shigongo wa Global Publisher akihojiwa na waandishi wa
habari, alisema ni kitu chema kufanya kazi yako kwa kumkumbuka Mungu
Ruge wa Clouds FM alisema, ni pengo kubwa sana kwani katika sanaa alikuwa anahitajika sana
HISTORIA FUPI YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA
HISTORIA YAKE:
Steven Charles Kanumbaa alizaliwa Januari 8, mwaka 1984 mkoani Shinyanga kabla ya umauti kumfiia Aprili 6, mwaka 2012.
Elimu ya msingi alipata katika shule ya Bugoyi, na baadaye akajiunga na
sekondari ya Mwadui, kabla ya kuhamia Dar Christian Seminary.
Baada ya kumaliza Kidato cha Nne Dar Christian, Kanumba alijiunga na
sekondari ya Jitegemee, Dar es Salaam pia kwa elimu ya Kidato cha Tano
na Sita.
Ni ni wakati huo akiwa Jitegemee Kanumba alianza shughuli za sanaa katika Kundi la Kaole Sanaa Group la Magomeni, Dar es Salaam.
Baada ya kukomaa Kaole, Kanumba aliamua kuanzisha kampuni yake mwenyewe
ya filamu na hadi anakutwa na umauti alikuwa mwigizaji anayefahamika
Afrika nzima.
Ameshirikiana na wasanii wakubwa duniani kama Ramsey Nouah wa Nigeria na amefanya kazi na mastaa wengine kadhaa wa Nigeria.
Miongoni mwa filamu ambazo alifanya ni Dar To Lagos, She is My Sister,
Ancle JJ, Oprah, Tufani, Johari, Gharika, Baragumu, Sikitiko Langu,
Dangerous Desire, Cross My Sin, Village Pastor, Family Tears na
kadhalika.
Hivi karibuni, alikaririwa akisema atagombea Ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
Kanumba atakumbukwa na wengi sana kwa ucheshi wake- upole na ushirikiano mzuri na wenzake katika kazi.
Kifo cha Kanumba ni pigo katika tasniya ya filamu Tanzania. Taifa
limempoteza mtu ambaye alikwishaanza kuitangaza vema nchi kupitia sanaa
hiyo na ambaye angetarajiwa kuitangaza zaidi katika anga za kimataifa
zaidi kupitia sanaa hii.
Nigeria sasa wanajua Tanzania sasa filamu. Nchi nyingi za Afrika zinajua sasa nah ii sehemu ya kazi nzuri kwa Kanumba.
Mwenyewe aliwahi kukaririwa alifika hadi Hollywood hadi Marekani, ambayo
ni ‘makka’ ya wacheza filamu. Kwa sasa mwili wa marehemu upo katika
hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment