Monday, February 27, 2012
WIZARA YA AFYA YAPOKEA MSAADA WA VIFAA VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYAWaziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda (wa pili kushoto) akipokea msaada wa vifaa vya kutolea huduma za afya zikiwemo dawa za kutibu ugonjwa wa kichocho na maabara ndogo za kubaini dawa zilizotengenezwa chini ya kiwango (dawa feki) kutoka Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Ujerumani ya MERCK inayoshughulika na utengenezaji wa dawa za binadamu,vifaa tiba na kemikali Dkt.Karl-Ludwig Kley leo jijini Dar es salaam. Vifaa hivyo vitasambazwa katika hospitali mbalimbali nchini na vituo vya afya vilivyo mipakani
Balozi
wa Ujerumani nchini Tanzania Klaus-Peter Brandes (kulia) akitoa
ufafanuzi kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda juu ya
dawa zilizotolewa leo jijini Dar es salaam na kampuni ya Ujerumani ya
MERCK inayoshughulika na utengenezaji wa dawa za binadamu,vifaa tiba na kemikali.Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Dkt. Peter Mmbuji.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda(katikati) akiwa na Kaimu
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Dkt. Peter Mmbuja wakifuatilia maelezo ya
kitabu cha mwongozo wa maabara ndogo inayohamishika ya kubaini dawa
zilizotengenezwa chini ya kiwango (dawa feki) yaliyokuwa yakitolewa na
balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Klaus-Peter Brandes.
No comments:
Post a Comment