Mzee wa Kimasai mkazi wa Longido akimshukuru na kumuombea dua njema Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete baada ya mzee huyo kukabidhiwa ng’ombe watano na mbuzi watano wilayani Longido jana.Mzee huyo ni mmoja wa wafugaji walipoteza mifugo yao yote kufuatia ukame mkali uliozikumba wilaya za Longido,Ngorongoro naMonduli.
Mwanafunzi Godlisten Ole Olais anayesoma kidato cha pili katika shule ya Sekondari ya Longido akiteta jambo na Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuwasili katika viwanja vya sekondari hiyo kuongoza uzinduzi wa wa mradi wa serikali wa uwezeshaji mifugo(seed stock) kwa kaya za wafugaji waliopoteza mifugo yote kutokana na ukame msimu wa 2008-2009 na 2009-2010 zilizofanyika wilayani longidojumapili.
Viongozi wa kabila la Kimasai(Laigwenani) wakimpa Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete zana za kijadi za uongozi mkuki na fimbo wakati wa hafla ya kukabidhi ng’ombe iliyofanyika wilayani Longido jumapili.
Viongozi wa kabila la Kimasai(Laigwenani) wakimpa Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete zana za kijadi za uongozi mkuki na fimbo wakati wa hafla ya kukabidhi ng’ombe iliyofanyika wilayani Longido jumapili
No comments:
Post a Comment